Writen by
sadataley
5:49 PM
-
0
Comments
JIANDAE KUPOKEA KUTOKA SHANGILIENI KWAYA ARUSHA
Baadhi ya waimbaji wa Tumaini Choir St. James Arusha wakiwa katika rekodi mkoani humo. |
Video hiyo ikikamilika itakuwa ni video ya tano ya kwaya hiyo ambayo ilitamba na video yao ya kwanza inayoitwa Shangilieni na kufuatiwa na Shangilieni part 2, video ya tatu Unishike huku video ya nne ni ya nyimbo za matumaini (Tenzi za Rohoni) ambayo walirekodi live na sasa wanaandaa ya tano itakayoitwa "Nisamehe.
Mambo yakipamba moto, hapana shaka wimbo huu ni Nisamehe |
Baadhi ya wababa wakirekodi wimbo wenye mahadhi ya mkoa wa Tanga, kama ilivyoada ya Tumaini mdumange haukosi. |
Kati ya mawazo bora ya sare ambayo Tumaini wamefaulu, kila mmoja kuvaa aina moja ya nguo lakini rangi rangi tofauti. |
Inapendeza kwakweli. |
Wakielezana jambo kabla hawajaendelea na rekodi. |
Hii ilikuwa nje ya majengo ya serikali mjini Pretoria Afrika ya kusini walipotembelea mwishoni mwa mwaka jana ambako ndiko walikoanzia kurekodi video hiyo. ©Samuel Kusamba. Habari na Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment