Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, January 27, 2014

Google yataka ufafanuzi kuhusu Udukuzi

Kampuni kubwa ya Google Imetaka uwazi kutoka kwa Rais Obama kuhusu pendekezo lake la kuzuia baadhi ya udukuzi unaofanywa na idara ya ujasusi nchini humo.
Kampuni ya Google inasema haifanyi udukuzi
Kufuatia ufichuzi wa aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya ujasusi nchini marekani,Edward Snowden,Rais Obama ameweka viwango vya utumizi wa data ya simu za watu.
Lakini afisa anayesimamia mswala ya sheria katika kampuni ya Google David Drummond ameiambia BBC kwamba Rais Obama anapaswa kutoa maelezo kuhusu viwango vya udukuzi huo katika mtandao.
Bwana Drummond amesema kuwa Marekani haifai kuchukua habari kwa wingi bali inafaa kutoa ombi la kupewa habari hizo kupitia agizo la mahakama.
Amesisitiza kuwa kampuni ya Google haina ushirikiano wowote na shirika lolote la ujasusi.
Bwana Drummond aliongeza kwamba serikali zote duniani zinapaswa kubuni sheria za kimataifa kuhusu udukuzi wa taarifa binafasi za watu kwenye internet.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment