Writen by
sadataley
11:58 AM
-
0
Comments
NDOA ZA JINSIA MOJA ZAKATALIWA KWA UMOJA CROATIA
![]() |
| Zoezi la kupiga kura likiendelea siku ya Jumapili nchini Croatia, ambapo 65% wamekataa ndoa za jinsia moja. ©AP |
Taifa la Croatia limepiga hatua kubwa katika kile kinachoelezwa kuwa ni kulinda maadili kama ambavyo Mungu alinuia, kufuatia siku ya Jumapili tarehe 1 Disemba, kupiga kura ya kukataa ndoa za jinsia moja, licha ya mataifa mengi ya barani Ulaya kukubaliana na ndoa za namna hiyo, na huku taifa hilo likiwa ni mwanachama mpya baada ya kujiunga mnamo Julai 2013.
Asilimia 65 ya waliopiga kura kuhusiana na jambo hilo, wamekubaliana na swali lililouliza kama wanaamini ndoa ni jambo linalohusisha mume na mke, huku asilimia 35 wakikataa - kwa maana nyingine wakiwa na mtaamo kuwa ndoa inaweza kuwa mwanaume kwa mwanaume ama mwanamke kwa mwanamke.
Tukio hili ambalo limezua gumzo kwa nchi wenza wanachama, litapelekwa sasa taifa la Croatia kuweka sawa katiba yao, na kukataza ndoa za jinsia moja, licha ya wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu kulaumu kuwa watu watakuwa wamenyimwa haki zao.
Kanisa Katoliki ambalo lilikuwa likisapoti kupingwa kwa ndoa za jinsia moja, liko katika furaha ya kupekee baada ya kufanikisha suala hilo kama ambavyo ndoto zao zilikuwa kwa taifa hilo lenye watu takribani milioni 4.4
"Ndoa ni muunganiko wa pekee ambao unawezesha kuzaliana", Kardinali wa taifa hilo, Josip Bozanic alisema katika ujumbe kwa wafuasi. Hii ndio tofauti ya kipekee kati ya ndoa na miunganiko mingine. Aliongeza Kardinali Bozanic
Juhudi za wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu zilianza kwa maandamano siku moja kabla, (Jumamosi), ambapo waliandamana kwenye mji mkuu wa taifa hilo, Zagreb - wakieleza kwamba watapiga kua ya hapana, ili ndoa za jinsia moja ziruhusiwe kikatiba.
Associated Press imeandika.

No comments
Post a Comment