Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Friday, December 6, 2013

‘Msihusishe takrima na uchaguzi 2015’


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Maombi, Kata ya Mbalizi, Mbeya Vijijini juzi. Picha na Bashir Nkoromo 
Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Mbeya. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewasihi viongozi wa kisiasa wanaotoa misaada kwa wananchi, katu wasihusishe na uchaguzi wa 2015 kwa kujenga mazingira ya kutaka kuonewa huruma.
Amesema, Serikali na wadau wote wa maendeleo wakiwamo wanasiasa hawana budi kutoa misaada kwa maendeleo ya taifa na wananchi bila kuwa na moyo wa kutaka kuonewa huruma katika masuala ya uchaguzi ama uongozi wa aina yoyote ile.
Kinana alisema hayo alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani hapa akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya jana.
“Viongozi wote, wakiwamo wa Serikali na CCM fanyeni kazi kwa kutekeleza dhamana kwa Watanzania na taifa kwa ujumla siyo kwa kujipanga,’’ alisisitiza.
Aliamua kutoa kauli hiyo baada ya mjumbe mmoja kwenye kikao hicho kumwomba akamweleze Rais Jakaya Kikwete arudi Mbeya kutembelea Saccos ambayo aliahirisha safari katika ziara iliyopita na kwamba asiporudi, atakosa kura katika uchaguzi ujao.
Katibu mkuu akiwa na sura ya ukali alisema viongozi wa CCM, lazima waonyeshe uongozi kwa kutoa ufafanuzi ulio sahihi na kwamba kamwe wasifanye mambo kwa kuogopa kupoteza kura wakati wa uchaguzi.
Aliwashauri viongozi wa CCM mjini hapa kujipanga upya na kuanza ukurasa wa kukijenga chama akisema kitendo cha kuwa na wanachama 24,000 kati ya watu karibu 400,000 ni dalili mbaya.
“Wakazi wa Mbeya wanaipenda Serikali na CCM, lakini walioharibu ni viongozi wenyewe wa CCM kwa kuendekeza majungu, upendeleo na ubaguzi katika utekelezaji wa kazi za chama,” alisema.
Kinana alionyesha kukerwa na kutofautiana kwa taarifa za CCM na Serikali katika wilaya hiyo akisema, lazima wawe makini na kuepuka kuandika vitu kwa ujumla ujumla. Jana jioni Kinana alitarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa eneo la Kiwanja cha Ruanda Nzovwe jijini Mbeya na leo anatarajia kuondoka mkoani hapa akielekea Wilaya ya Makete mkoani Njombe.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment