Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, December 2, 2013


Marais wa nchi wanacham wa EAC wasaini mkataba wa kuanza mchakato wa kuwa na sarafu moja

Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Na Flora Martin Mwano
Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wamesaini mkataba wa kuanza mchakato wa kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanchama wa jumuiya hiyo. Sherehe za kutia saini mkataba huo zilifanyika jana jumamosi jijini Kampala nchini Uganda ambako viongozi wa Mataifa matano wanachama walikutana.

Marais wa Mataifa ya EAC, Yoweri Mseveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkuruzinza wa Burundi walihudhuria kikao cha 15 cha umoja huo ambacho kilichofikia maamuzi hayo jana jumamosi.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa EAC Richard Sezibera alisema hatua hiyo inathibitishauanzishwaji wa matumizi ya sarafu moja mara mchakato wa maandalizi utakapokamilika na hii ni hatua mojawapo ya kuhakikisha nchi za EAC zinafikia azimio la kuwa na shirikisho la kisiasa ambalo ni hatua ya juu kabisa.
Umoja wa sarafu ni miongoni mwa malengo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC, mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imeanza kutekelezwa.
Katika kikao hicho cha Kampala Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alichukua uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Aidha viongozi hao walikubaliana watakuwa wanashauriana mara kwa mara kuhusu maswala muhimu yanayohusu jumuiya nzima ya EAC.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment