Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, November 24, 2013

Misri yamtaka balozi wa Uturuki kuondoka

Misri imemtaka balozi wa Uturuki nchini humo kuondoka mara moja na kuvunja mahusiano ya kidplomasia na taifa hilo,Katika kile ambacho serikali ya Misri imesema kuwa Uturuki kuitaka Misri kumuachia huru rais aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi..

Wafuasi wa Mohamed Morsi
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema kuwa inavunja uhusiano wa kidiplomasia na Uturuki kutokana na hatua ya taifa hilo kuingilia maswala ya ndani ya Misri.
Kumekuwa na mvutano kati ya mataifa hayo mawili huku Uturuki ikiikosoa Misri kwa hatua yake ya kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mapema mwaka huu.
Nchi hizo mbili zilivunja mahusiano ya kibalozi mara baaada ya jeshi kumuondoa madarakani rais Morsi,na balozi wa Misri nchini Uturuki alirejea Cairo,licha ya mwenzake wa Uturuki kutoondoka kurudi Ankara, hivyo serikali ya kijeshi iliyoko madarakani imesema ni lazima balozi huyo aondoke ndani ya mipaka ya taifa hilo kwa kuwa nchi yake inataka kupinga maoni na mawazo ya watu wa misri.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment