Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, November 24, 2013

Makamba, Tido, Zitto waula TFF

Rais Mpya wa TFF Jamal Malinzi akizungumza na waandishi wa habari 
Na Vicky Kimaro, Mwananchi
Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limevitaka vyama wanachama wake kufanya marekebisho ya katiba zao kwa kuingiza kipengele cha Kamati ya Maadili ya rufaa ili  kushughulikia masuala yote ya maadili ndani ya vyama vyao wakati ile ya Maadili ya Rufaa itakuwa ya mwisho katika kutoa uamuzi.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi mbali na vyama wanachama wake kuingiza kipengele hicho pia ametangaza wajumbe wa kamati ndogo ndogo za shirikisho hilo, wakati zile za haki na uchaguzi atazitangaza baadaye.
Malinzi amefikia uamuzi huo baada ya kuvunja kamati zote za TFF mara baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha uchaguzi kilichofanyika hivi karibuni na kumshinda mpinzani wake, Athuman Nyamlani.
Kamati alizotangaza Malinzi ni ile ya Habari na Masoko ambayo imejaa vigogo ikiongozwa na Hamad Yahya ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi huku Makamu wake akiwa Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba wakati wajumbe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd,  Tido Mhando.
Wengine ni mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, na katibu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ambaye atachaguliwa.
Pia, ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji ambao ni  Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk Paul Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuyava.
Geofrey Nyange ‘Kaburu’ anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald Yambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
Kamati ya Ufundi inaongozwa na Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi ‘Zamunda’, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk Cyprian Maro.
Kamati ya Soka la Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud ‘Maestro’.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake  wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.
Dk Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk Mwanandi Mwankemwa, Dk Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment