Writen by
sadataley
3:03 PM
-
0
Comments
Mahakama ya juu nchini Guinea imeridhia matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwezi september ambapo chama cha rais wa nchi hiyo Alpha Conde kilishinda.

Kura zikihesabiwa kwenye uchaguzi nchini Guinea
Mahakama imetupilia mbali maombi ya upinzani waliotaka matokeo ya uchaguzi huo yabatilishwe.
Chama cha Rais Conde Rally of Guinean People RPG kilishinda viti 53 katika uchaguzi huo, japo hakikufanikiwa kuwa na wingi wa wabunge ili kufanya ushawishi katika bunge la nchi hiyo lenye wabunge 114.
Mpinzani wa karibu wa Rais Conde, Cellou Dalein Diallo na chama chake cha UFDG kilishinda viti 37 huku chama cha Waziri Mkuu wa zamani Sidya Toure cha UFR kikipata viti 10. Viti vingine vilivyobaki vilichukuliwa na vyama vidogo vidogo 12 vya nchi hiyo. Na kutokana na matokeo hayo upo uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto.
Kwa mujibu Rais wa Mahakama ya juu katika hukumu yake alisema hakuna hata dai moja la walalamikaji lililokuwa na ushahidi wa kutosha.
Msemaji wa mwamvuli vyama vya upinzani amesema wamesikitishwa na uamuzi huo wa mahakama na kusema kwa sasa wanaendelea na mazungumzo ili kujua ni hatua gani watakazozichukua.
Uchaguzi huo wa wabunge ni kwanza kufanyika nchini humo tangu yalipofanyika mapinduzi mwaka 2008. Uchaguzi wa wabunge umekuwa ukihairishwa mara kwa mara kutokana na ukosefu wa usalama nchini humo.
Waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi huo ulikuwa umegubikwa na kasoro kadhaa.
No comments
Post a Comment