Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, November 20, 2013

Je wakimbizi Dadaab watarejea Somalia?

Umoja wa Mataifa unajiandaa kuanza utafiti kwenye kambi kubwa ya wakimbizi duniani ya Dadaab iliyopo Kaskazini mwa Kenya ili kujua wakimbizi karibu nusu milioni kutoka Somalia waliopo kwenye kambi hiyo ambao wapo tayari kurejea nchini mwao.
Wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
Wiki iliyopita Kenya na Somalia walitiliana sahihi makubaliano na Umoja wa Mataifa ili kuanza kurejesha wakimbizi hao nchini Somalia.
Mwandishi wa Habari wa BBC aliyepo kwenye kambi hiyo anasema ni wakimbizi wachache chini ya mia moja ambao wapo tayari kurejea nchini mwao, ambapo wengi wanasema hali ya usalama nchini Somalia bado ni hatari kutokana na kuwepo kwa wapiganaji wa Kiislamu.Kuwepo kwa wakimbizi imezusha wasiwasi wa kisiasa nchini Kenya kufuatia shambulio la Septemba ambapo wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni wa Kisomali kushambalia kituo cha biashara cha Westgate ambapo watu 67 waliuawa.
Serikali ya Kenya imesema miaongoni wa walioendesha shambulio hilo ni wakimbizi kutoka kwenye kambi hiyo ya Daadab.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment