Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, October 31, 2013

Wakenya washinikiza wabakaji wakamatwe

Mamia ya waandamanaji nchini Kenya wamewasilisha kwa polisi hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka msichana huyo wa miaka 16.
Liz alibakwa na watu waliomtupa kwenye shimo la choo na kumvunja uti wa mgongo
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume na kutupwa katika shimo la choo ambapo alivunjika uti wa mgongo wake.
Wanaume wanaotuhumiwa kumbaka msichana huyo waliamrishwa na polisi kukata nyasi kama adhabu ya kitendo hicho.
Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.
Waandamanaji hao wameelezea kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili kumtendea haki msichana huyo.
Pia wanataka polisi waliowaadhibu washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.
Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.
Kampeini hii imekuja baada ya msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.
Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment