Writen by
sadataley
7:45 PM
-
0
Comments
Wizara ya sheria nchini Burundi imetangaza kumuachia huru mwandishi wa habari Hassan Ruvakuki ambaye awali alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za uhaini.
Taarifa zaidi zinasema Hatua ya kumwacha Huru Mwanahabari huyo Hassan Ruvakuki imetolewa na wizara ya Sheria nchini Burundi.
Shirika la waandishi wa Habari wasio na mipaka limesema kuwa limefura hishwa na Hatua hiyo na kwamba itaongeza uaminifu zaidi katika utendaji wa kazi ya uandishi habari nchini Burundi.
Ruvakuki alikamatwa mwezi Novemba mwaka jana akituhumiwa kushiriki katika kundi la uasi nchini Burundi, kundi ambalo liliendesha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali katika mkoa wa Cankuzo mpakani na Tanzania.
Ruvakuki alihukumiwa kifungo cha maisha mwezi June mwaka jana na baadaye mwezi januari mwaka huu kifungo chake kikapungua hadi miaka mitatu baada ya kukata rufaa.
No comments
Post a Comment