Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, October 24, 2013

Mizizi ya Al Shabaab UK yafichuliwa

Shirika la habari la BBC limegundua kuwa takriban watu 50 kutoka Uingereza wana uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Shabaab na makundi mengine husika
Al shabaab wamekiri kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya wiki nne zilizopita
Wengi walio kwenye orodha hiyo walisafiri kwenda nchini Somalia kupigana kwa niaba ya kundi hilo na wengine kujaribu kuifanya safari hiyo ingawa hawakufanikiwa.
Al Shabaab, ambao makao yao makuu ni Somalia walikiri kuhusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jengo la kifahari la Westgate mjini Nairobi.
Mawakili wa familia ya kiingereza ya mmoja wa watu waliosajiliwa kupigania Al shabaab ingawa kauwa baadaye, wanachunguza kifo chake.
Majina 47 yaliyokusanywa na BBC yalitoka kutoka kwa watu mbali mbali ikiwemo stakabadhi za mahakamani.
Takriban watu 32 kati ya walio kwenye orodha hiyo , wanashukiwa kujiunga na al-Shabaab ili kupigana , wakati majasusi wa Marekani M15 walipowanasa wengine wakijaribu kusafiri kwenda Somalia.
Wengine saba walitajwa katika mahakama za Uingereza kwa kujaribu kwenda Somalia ingawa njama yao ilijulikana na kutibuliwa.
Hali ya washukiwa hao haijulikani lakini wanne bila shaka wameuawa.
Ni pamoja na Tufail Ahmed kutoka Mashariki mwa London. BBC imegundua kuwa polisi waliifahamaisha familia yake kwua alifariki akiwa nchini Somalia mwezi Novemba mwaka jana.
Familia yake imelitaka shirika lisilo la kiserikali la charity Reprieve kuchunguza madai kuwa majeshi ya nchi za Magharibi yalihusika na mauaji hayo,.
Wizara ya ulinzi imekataa kuzungumzia swala hilo.
Wengine walishtakiwa kwa kuchangisha pesa kwa niaba ya al-Shabaab, au kufanya mipango ya kuwasafirisha
Wanne kati ya wanaume hao wamefariki wakiwemo wanaume walioonekana kwenye kanda ya video iliyotolewa na al-Shabaab wiki moja iliyopita.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment