Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, October 28, 2013

Madagascar:Uchaguzi huru na wa haki

Matokeo ya mwanzomwanzo yanaonyesha mshirika wa rais aliyeng’olewa madarakani Marc Ravalomanana akiwa mbele kwa hesabu za kura.
Richard Jean-Louis Robinson ana asilimia 30 ya kura hadi sasa huku mshindani wake, Hery Martial Rakotoarimanana Rajaonarimampianina akipata asilimia kidogo zaidi ya 15%.
Matokeo rasmi huenda yakajulikana baada ya wiki moja.
Ikiwa hakuna mgombea yeyote atapata zaidi ya asilimia 50, ya kura zilizopigwa, duru ya pili itafanyika tarahe 20 Disemba.

Shughuli ya kuhesabu kura inaendela na huenda ikamalizika baada ya wiki moja
Waangalizi wa kimataifa wameutaja uchaguzi wa urais nchini Madagascar kuwa huru na wa haki huku matokeo ya uchaguzi huo yakiendelea kusuburiwa.
Uchaguzi wenyewe uliofanyika siku ya Ijumaa ulikuwa wa kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika kisiwani humo mwaka 2009.
Mkuu wa uangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya, Maria Muniz de Urquiza, amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki licha ya visa kadhaa vya ghasia.
Naye Nandi-Ndaitwah, mwangalizi mkuu wa uchaguzi kutoka kanda ya Afrika Kusini, alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wenye amani , wazi na kuwa unaonyesha matarajio ya watu.
Wagombea wakuu wawili, wameahidi kuujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka mingi ya vurugu za kisiasa.
Zaidi ya 92% ya watu milioni 21 nchini humo wanaishi kwa dola mbili kwa siku , kulingana na benki ya dunia.
Bwana Rajaonarimampianina amesema kuwa ana nia ya kuwasaidia vijana wasio na ajira , kujenga upya miundo msingi na kuimarisha kilimo , kufanya mageuzi katika sekta ya elimu pamoja na kuimarisha demokrasia nchini humo.
Bwana Robinson anasema kuwa mpango wake wa maendeleo unatokana na ule wa Rais wa zamani Bwana kujaribu kujenga upya sekta ya utalii inayokumbwa na changamoto si haba nchini humo.
Madagascar imekuwa ikikumbwa na vurugu za isiasa tangu mwaka 2009, wakati Andry Rajoelina alipompindua kutoka mamlakani, aliyekuwa Rais Marc Ravalomanana.
Mapinduyzi ya kijeshi yalisababisha nci hiyo kutengwa na jamii ya kimataifa, na hata kunyimwa misaada.
Lakini mapema mwaka huu Bwana Rajoelina na Ravalomanana walikubali kutoshiriki uchaguzi mkuu kulingana na mpango ulioafikiwa na muungano wa SADC.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment