Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Monday, October 21, 2013

Kenya itaingilia kati kujihami

Rais wa Kenya anasema nchi yake huenda ikabidi 'kuingilia kati nje' ili kuilinda Kenya na majirani zake.
Rais  Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta amesema hayo karibu mwezi baada ya shambulio katika jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi ambapo watu kama 67 waliuwawa.
Wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabab, wamedai kufanya shambulio hilo.
Kenya tayari ina wanajeshi wanaopigana na Al Shabab nchini Somalia.
Rais Kenyatta alisema Kenya iko tayari kuchukua hatua wakati wowote inapohitajika, ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Alisema Wakenya wataimarisha usalama nyumbani, kwa kuwa waangalifu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment