Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 6, 2013

JUHUDI ZA AMANI ZASHIKA KASI MISRI

Wafuasi wa Mohammed MorsiMaseneta wawili wa Marekani John McCain na Lindsey Graham wamewasili mjiniCairo, wakati jitihada zikishika kasi kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Misri uliozuka baada ya kupinduliwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi.

Wasiwasi unazidi kutanda baada ya serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi kutangaza mpango mpya wa kuyasitisha maandamano, ambako wafuasi wa Morsi wanataka arudishwe madarakani.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wageni mashuhuri wa kiimataifa wanaozuru Misri, wanaotarajia kusaidia kusimamia kupatikana suluhu ya amani katika hali ya suitofahamu iliopo kati ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa na serikali inayoungwa mkono na jeshi.
Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu hatua zilizopigwa.
Kwa wakati mmoja kulikuwa na ripoti kwamba baraza jipya la mawaziri lilikuwa tayari kuwaachia viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood kutoka gerezani na kuwapatia nyadhifa za mawaziri iwapo watasitisha maandamano mjini Cairo.
Hata hivyo mshauri wa rais amekana tuhuma hizo na wafuasi wa Morsi wamesisitiza hawatokubali chochote isipokuwa kurudishwa Morsi madarakani.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment