Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 19, 2013

Watakiwa kuachana na siasa ofisini

Na Jackline Masinde
Geita.Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Taifa (Tughe),Ally Kiwenge amewataka wafanyakazi wa Serikli mkoani humo kuacha kujiingiza katika siasa kwa madai kufanya hivyo kunatishia kuharibu utendaji kazi zao.
Kauli hiyo ilikuja baada ya wafanyakazi wa sekta ya afya na halmashauri ya wilaya kuwa na mgogoro na waajiri wao hali iliyosababisha kuzorota kwa utendaji kazi jambo linalowaumiza wananchi wasio katika mgogoro huo.
Akizungumza jana na watumishi hao pamoja na waajiri wao katibu huyo alionya kuhusu kuingiza masuala ya kisiasa katika utendaji kazi na kudai kuwa unachangia kuharibu mfumo wa kazi sambamba na kuleta makundi na mogogoro isiyona tija huku wachache wasiokuwamo katika makundi hayo huumia na hali hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment