Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 18, 2013

WAAFRIKA WAKOSOA MAHAKAMA YA ICC

icc ea749
WAZIRI wa sheria wa Rwanda anasema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC hulenga  kundi fulani kwa misingi ya ubaguzi katika utendaji kazi zake. Matamshi yake yalitolewa  wakati  mahakama hiyo ikiadhimisha ya miaka 15 tangu ilipobuniwa.  Alisema hivi leo Waafrika  wengi  wanajiuliza  ikiwa  bara la Afrika lina haja tena na mahakama  hiyo ya ICC. (HM)

Mnamo Julai 17 mwaka wa 1998 wajumbe katika mkutano wa kimataifa mjini Roma walipiga kura kubuni mahakama hiyo kama hatua ya mwisho ya kulinda haki kwa kushtaki na kusikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu mwingine ambao mahakama za vyombo vya dola zinashindwa kukabiliana nayo au hazina uwezo wa kuchukulia hatua za kisheria.

Kwa sasa mahakama hiyo ya kimataifa yenye makao yake The Hague, ina kesi  zinazohusu nchi 8 za Afrika ikiwemo Kenya, Sudan na Ivory Coast.
Rwanda ni mojawapo ya nchi zilizokataa kutia saini mkataba huo wa Roma na ni mkosoaji mkubwa wa mahakama hiyo ya ICC.

Waziri wa sheria wa  Rwanda Johnston Busingye aliiambia sauti ya Amerika kwamba hata ingawa Rwanda inaunga mkono  dhana ya sheria za kimataifa, anahisi kwamba mahakama ya ICC inawalenga Waafrika pasipo haki.

Kote barani Afrika, uungaji mkono wa mahakama ya ICC unafifia. Mnamo mwezi Mei Umoja wa Afrika ulipiga kura kurejesha kesi  dhidi ya rais wa Kenya na naibu rais  nchini Kenya kutoka ICC. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliishtumu ICC kwa ubaguzi wa rangi. Mahakama  hiyo inakanusha kuwa inawalenga Waafrika.

Na katika kura ya maoni iliyofanywa na wananchi wa Kenya, asili mia 39 walisema wanaunga mkono kesi dhidi ya rais wao na naibu wake kusikilizwa na ICC, lakini asili mia kubwa zaidi ya wakenya wanataka  kesi hizo zirejeshwa nchini Kenya au zifutwe kabisa.

Rais wa Kenya bw. Uhuru Kenyatta na Naibu rais  bw. William Ruto wameongoza kampeni kali dhidi ya ICC. Lakini mahakama hiyo inasema kesi dhidi yao zitaanza baadaye mwaka huu.
Chanzo: Voaswahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment