Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 17, 2013

SIMANZI FAMILIA ZA ASKARI JWTZ.

Familia za askari leo huko Songea zaungana kwa majonzi na masikitiko makubwa katika kuiaga miili ya waliofariki katika jimbo la Darful nchini Sudani.

Kepteni John Kivunge wa JWTZ akitangaza ratiba ya tukio la kuwaaga askari wa Tanzania waliofariki katika Jimbo la Darfur nchini Sudan. 
Songea. Vilio na simanzi vimetawala katika baadhi ya familia za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao waliuwawa katika eneo la Darfur, Sudan ambako wanashiriki katika ulinzi wa amani.
Mamia ya waombolezaji walionekana katika makazi ya familia za marehemu; Songea mkoani Ruvuma na Nachigwea mkoani Lindi ambako ziko kambi ambazo baadhi ya askari hao walikuwa wakifanya kazi.
Imefahamika kuwa wanajeshi waliouwawa Jumamosi iliyopita wanatoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea,  44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es Salaam.
Jana gazeti hili lilibaini kuwapo kwa maombolezo katika baadhi ya familia za wanajeshi hao baada ya kupokea taarifa za vifo vyao kutoka JWTZ. Hata hivyo bado majina ya waliofariki hayajawekwa hadharani.
Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe juzi aligoma kutaja majina hayo akisema kuwa majina hayo hayajatolewa rasmi na kwamba familia za marehemu zilikuwa hazijajulishwa.
“Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alisema Kanali Mgawe.
Hata hivyo kupitia katika maeneo ilikokuwa misiba hiyo jana, gazeti hili lilifanikiwa kufahamu majina ya baadhi yao, ambayo yanafanana na yale yaliyotangazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya magazeti.
Katika Kambi ya Chabruma, Songea mkoani Ruvuma kulikuwa na umati wa waombolezaji nyumbani kwa mmoja wa wapiganaji hao, Koplo Oswald Chaula ambaye alikuwa katika Kikosi cha Mizinga Chabruma na ndugu zake walikiri kupokea taarifa za msiba huo.
Hali kama hiyo ilikuwa nyumbani kwa Koplo Mohamed Chukilizo katika Kambi ya Majimaji, Nachingwea ambako baadhi ya ndugu na jamaa za zake wakiwamo mkewe na baba mkwe wake walikutana jana jioni kujadiliana kuhusu msiba.
Mwananchi pia lilishuhudia waombolezaji wakiwa wamekusanyika eneo la Mjimwema, Songea Mkoani Ruvuma ambako ni nyumbani kwa Komandoo Rodney Ndunguru aliyetoka kikosi cha 92KJ Ngerengere, Morogoro, baada ya kupokea taarifa za msiba huo. 
Vilio, Simanzi
Katika kambi ya Chabruma, mke wa marehemu Koplo Oswald aliyejitambulisha kwa jina la Maria alikuwa akilia kwa simanzi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa waliofariki ni baba watoto wake.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment