Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, July 14, 2013

Kuelekea Ukingoni mwa Mpango wa Maendeleo Duniani (Millenium Development Goals) Hali ya Chakula Afrika bado inatisha

Mboga na matunda
Ni nchi saba tu kati ya nchi 53 za Umoja wa Afrika ambazo ziliahidi kutenga takriban asilimia 10 ya bajeti yake ya kitaifa kuwekeza katika kilimo na kufikia malengo yao.
Mashirika ya kutoa misaa yanasema uwekezaji katika kilimo ndiyo chanzo muhimu cha kuvunja ukosefu wa usalama wa chakula katika eneo la Afrika Magharibi.

Na huku maadhimisho ya miaka  kumi ya makubaliano hayo yakisherehekewa wiki hii mashirika fadhili yanataka nchi za Umoja wa Afrika kutimiza ahadi waliotoa katika mkutano wa Maputo.

Mnamo mwaka wa 2003, viongozi wa nchi 53 za Afrika walikubaliana kutenga takriban asilimia 10 ya bajeti zao za kitaifa kuwekeza katika sekta ya kilimo na mifugo  ifikapo Julai  2008.

Lakini miaka 10 baadaye ni Burkina Faso, Niger, Guinea, Mali , Malawi na Ethiopia zilizofikia lengo hilo. Nchi nyingi kama vile Nigeria, Guinea Bissau na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo zimetenga asilimia 3 tu ya bajeti yake kwa uwekezaji wa kilimo.Hii ni licha ya kwamba wakulima wenye mashamba madogo wanawakilisha asilimia 80 ya raia wao.
habari kwa hisani ya Sauti  ya Amerika
http://www.voaswahili.com/content/hali-ya-chakula-afrika
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment