Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 8, 2013

Hatimaye Abu Qatada afikishwa Jordan

Mahakama nchini Jordan imeshitaki Muhubiri wa Kiislamu Abu Qatada kwa makosa yanayohusiana na Ugaidi baada ya kurejeshwa nchini Humo akitokea Uingereza mapema hii leo.
Mashitaka ya kesi hiyo yamefuata yale ya mwaka 1999 dhidi yake.Amesalia kwenye kizuizi chini ya gereza lenye ulinzi mkali kwenye eneo la jangwa nje kidogo ya mji mkuu wa Amman.
Kufika kwa Abu Qatada nchini Jordan kumemaliza mabishano ya kisheria ya miaka nane ya serikali ya Uingereza kutaka kumrejesha nchini Jordan,
Mabishano ambayo yameigharimu serikali ya Uingereza kiasi cha pound milioni mbili na nusu fedha za walipa kodi.
Mwandishi wa BBC mjini Amman amesema licha ya ahadi ya serikali ya Jordan ya kuendesha kesi hiyo kwa uwazi na usawa, lakini wanahabari wamezuiliwa kuingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
chanzo: bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment