Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 8, 2013

Hali ya taharuki yatanda nchini Misri

Maafisa wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300 wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia. Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.
Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.
Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.
Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.
Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.
Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.
Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jeshi.
habari toka bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment