Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 17, 2013

HALI NI TETE HUKO KENYA, SHULE ZA MSINGI ZAFUNGWA.

Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za msingi za umma kufuatia mgomo wa walimu ulioingia wiki ya nne sasa.

Wanafunzi Kenya
                                                         Wanafunzi nchini Kenya wakiwa darasani
Waziri wa elimu Prof. Jacob Kaimenyi amesema kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ameshutumu walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.
Zaidi ya walimu laki mbili na arobaini wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakidai nyongeza ya asili mia mia tano ya mishahara waliyoahidiwa na serikali mwaka wa 2007.   Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya usafiri, ya nyumba na matibabu. Serikali imesema kuwa wazazi wataarifiwa juu ya siku ya kufunguliwa tena shule.
Waziri huyo wa elimu Pro. Kaimenyo amesem akuwa wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nane wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya miezi minne ijayo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment