Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 10, 2013

Baraza la mawaziri kuundwa Misri

Waziri mkuu mpya wa Misri,Hazem al-Beblawi anaanza kibarua cha kuteua baraza la mawaziri , wiki moja baada ya kuondolewa mamlakani kwa rais Mohammed Morsi.
Waombolezaji wakipiga mayowe kando ya gali liliokuwa limebeba maiti ya polisi aliyeuawa kwenye ghasia
Hii ni katika hatua ya kujaribu kuleta maridhiano na Hazem El Beblawi amesema atatoa viti vya uwaziri kwa vuguvugu la Muslim Brotherhood linaloongozwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wakuu wa vuguvugu hilo ameiambia BBC kwamba hawatashiriki katika serikali yoyote hadi pale kiongozi wao Mohammed Morsi atakaporejeshwa mamlakani.
Taarifa hiyo inajiri wakati ambapo Jeshi la Misri limeonya dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga kipindi hicho cha mpito.
Bwana Beblawi anatarajiwa kutoa nafasi za kazi za uwaziri kwa vuguvugu hilo licha ya kusema kuwa haliko tayari kushirki katika serikali ya mpito kufuatiua hatua wanayosema ni ya jeshi kumpindua Morsi.
Brotherhood wamesema hawataunga mkono mpango wa serikali hiyo kuandaa uchaguzi mpya hadi pale mageuzi yatakapofanyika.
Marekani imesema inaunga mkono ingawa kwa makini hatua ya kukupendekeza mageuzi.
Ratiba iliyotolewa ya maandalizi ya uchaguzi mpya, ilitangazwa na rais wa muda, Adly Mansour siku ya Jumatatu masaa kadhaa baada ya angalau watu 51 kuuawa wengi wao wakiwa wa chama cha Muslim Brotherhood. Waliuawa wakiwa nje ya kambi ya jeshi wanakoamini kuwa Morsi anazuiliwa
Amri ya rais wa mpito inalenga kubuni jopo maalum litakalofanyia katiba marekebisho katika kipindi cha wiki mbili.
Huku watu wakiendelea kuvutana , hofu nayo inaongezeka sio tu kuhusu kuokoa mapinduzi bali nchi nzima.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment