Writen by
sadataley
7 years ago
-
0
Comments
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema kuwa, askari wa Rwanda waliokamatwa mwishoni mwa juma lililopita katika mkoa wa Kivu Kaskazini watakabidhiwa mamlaka husika ili waweze kurejeshwa nchini Rwanda.
Kwa mujibu wa duru za habari, askari wawili wa Rwanda walikamatwa na silaha na vifaa vya mawasiliano usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu karibu na uwanja wa ndege wa Goma mashariki mwa Jamhuri yya Kidemokrasia ya Congo.
Meja Guillaume Ndjike, mmoja wa wasemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mkoa wa Kivu Kaskazini
Kwa mujibu wa Meja Guillaume Ndjike, mmoja wa wasemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, askari hao wa Rwanda watakabidhiwa kwa tume ya pamoja yenye dhamana ya kukagua mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Taasisi hii itahusika na kukabidhi askari hawa kwa serikali ya Rwanda, amesema msemaji huyo wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Meja Ndjike aidha ameiomba nchi jirani ya Rwanda nayo kutumia utaratibu huo wakati askari wake wanapokuwa kwenye ardhi yake.
Kumekuwa na mvutano kwa miaka kadhaa kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Kinshasa imekuwa ikimtuhumu jirani yake huyo kwamba, amekuwa akisaidia makundi ya watu wenye silaha nchini humo.
Hata hivyo serikali yya Kkigali imekuwa ikkikanusha tuhuma hizo na kusisitiza kwamba, haihusikki kwa namna yoyote na machafuko yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Parstoday
No comments
Post a Comment