UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18 NOW OPEN! DEADLINE 30/03/2018 CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More
menu
Dropdown Menu
Thursday, July 4, 2019
Unene 'unasabisha saratani kuliko uvutaji sigara' kwa watu wengi
Writen by
sadataley
2:42 PM
-
0
Comments
Unene kwa sasa
umekuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza
kuliko uvutaji sigara, taasisi ya saratani nchini humo imeeleza.
Taasisi
ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo,
ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta
tumbaku.
Inasema mamilioni wako hatarini kuugua saratani kwasababu
ya uzito na kuwa watu wenye uzito mkubwa huzidi idadi ya wavuta sigara
kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.
Lakini matangazo ya mabango ya kampeni kuhusu unene na hatari ya kupata saratani yamekosolewa kwa kujeli watu wanene. Si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kushutumiwa
kukejeli watu wanene. Wengine wakisema kuweka tangazo hilo kama vile
matangazo ya pakiti za sigara si jambo zuri.
Lakini taasisi hiyo imejitetea kuwa haiwalaumu watu walio na uzito mkubwa.
Wala
haisemi kuwa uvutaji wa sigara ni sawa na kuwa na uzito mkubwa
wakihusisha na hatari ya kupata saratani. Vyote viwili vinahatarisha
afya.
Lakini taasisi hiyo imesema uzito mkubwa au unene
husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na
uvutaji wa sigara unasababisha watu 54,300 kuugua saratani.
Lakini wakati idadi ya wavuta sigara ikipungua, idadi ya watu wenye uzito mkubwa inaongezeka, suala la kushughulikiwa.
Wakati uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani ukibainishwa vyema, kibaiolojia bado haijaeleweka vyema
Kuwa
na uzito mkubwa au mnene haimaanishi kuwa lazima mtu huyo apate
saratani, lakini mtu huyo anaongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.
Ongezeko la hatari hujitokeza zaidi iwapo mtu ataongezeka uzito zaidi.
Kwa
mujibu wa watafiti saratani mbalimbali zinahusishwa na uzito mkubwa:
Saratani ya matiti kwa wanawake waliokoma hedhi (menopause), utumbo,
ini, saratani ya damu, saratani ya ubongo, koo, tezi, figo, kongosho,
tumbo,ovari.
Uhusiano kati ya unene na saratani ni kwa watu wakubwa pekee, ingawa kwa watoto wadogo ni muhimu kuwa kwenye tahadhari pia.
No comments
Post a Comment