UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Saturday, March 31, 2018

Simba kuweka kambi Iringa kuwawinda Njombe Mji


Simba SC wameondoka asubuhi ya leo majira ya saa moja kuelekea Iringa kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya safari ya Njombe kwa ajili ya mchezo wa ligi.

Kikosi hicho kitaweka kambi Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na Njombe Mji kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo ya ligi, itachezwa Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe huku wenyeji wakiwa wametoka kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Stand United jana.

Wekundu hao wa Msimbazi wataondoka Iringa Jumatatu ya wiki lijalo kuelekea Njombe, tayari kwa mchezo huo utakaopigwa siku ya Jumanne.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment