Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 20, 2018

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy azuiliwa na polisi

Ex-French President Nicolas Sarkozy (file pic)

Haki miliki ya pichaAFP
Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anazuiliwa na polisi akihojiwa kuhusu tuhuma kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Polisi wanachunguza tuhuma hizo kuhusiana na ufadhili wa fedha alizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.
Polisi waliwahi kumhoji awali.
Msaidizi wake wa zamani Alexandre Djouhri pia alikamatwa jijini London karibuni.
Bw Sarkozy alishindwa katika juhudi zake za kutaka kurejea madarakani mwaka 2012.
Duru kutoka kwa mahakama zimesema rais huyo wa zamani alikuwa anahojiwa Nanterre, magharibi mwa Paris.
Mwaka 2013, Ufaransa ilianzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba kampeni ya Sarkozy ilipokea mchango kutoka kwa hazina ya pesa haramu za Gaddafi.
Bw Sarkozy amekanusha tuhuma hizo.
Duru zinasema mmoja wa mawaziri wa zamani wa Sarkozy na ambaye ni mshirika wake wa karibu Brice Hortefeux pia alihojiwa na polisi Jumanne.
Tuhuma hizo zilitolewa na mfanyabiashara Mfaransa mwenye asili ya Lebanon Ziad Takieddine na baadhi ya maafisa wa zamani wa Gaddafi.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment