Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 20, 2018

Kikosi cha Simba SC chapewa mapumziko


Kikosi cha wachezaji soka nchini Tanzania, Simba kimepewa mapumziko mafupi ya kutofanya mazoezi ya aina yeyote kuanzia leo kwa lengo la kuweka viungo vyao sawa baada ya kurudi nchi kutokea katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Hayo yameelezwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo asubuhi ya leo kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuweza kuwapa muda mzuri wachezaji wao wa kupumzika ili waweze kujiweka sawa katika kujiandaa na michezo inayofuata kwenye ligi kuu Tanzania Bara inayoendelea kurindima katika baadhi ya viwanja.

"Kikosi cha Simba kimepewa mapumziko mafupi ambapo kitaanza tena mazoezi Jumamosi kujiandaa na michezo inayofuata kwenye ligi kuu Tanzania Bara", imesema taarifa hiyo.

Simba kwa sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na alama 46 sawa na watani wao wa Jadi Yanga zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa pamoja na idadi ya michezo Yanga ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment