Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 19, 2018

Rais Pierre Nkurunzinza atia saini sheria marekebisho ya katiba

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza jana ametia saini sheria tata inayotoa wito kwa wananchi wa taifa hilo wenye umri wa kupiga kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba ambayo yanaweza kumruhusu kuendelea kukaa madarakani hadi mwaka wa 2034 kushiriki kwenye kura hiyo.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae yupo madarakani tangu mwaka 2005, sasa anataka kuendelea kusalia kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2035.

Sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba ya Burundi inasema mabadiliko yataidhinishwa iwapo asilimia 50 ya kura za ndio na kura moja itafikiwa.

Hata hivyo upinzani unasema alichokifanya rais Nkurunziza kinakwenda kinyume na katiba ya nchi, maana mabadiliko ya katiba ili yaidhinishwe, lazima yapitie katika mabaraza ya bunge na seneti.

Wale wote wanaohitaji kuendesha kampeni ya ndio au hapana kuhusu mabadiliko ya katiba wamepewa muda wa hadi April 6 kujiorodhesha kwa tume ya uchaguzi ambapo kampeni imepangwa kuanza majuma mawili kabla ya terehe ya kupiga kura.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment