Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 19, 2018

Dunia yakabiliwa na upungu wa maji safi - UNESCO

Ongezeko la idadi ya watu, kubadilika kwa lisha pamoja na maendeleo yamepelekea kuwepo upungufu wa maji safi duniani. 
Ripoti ya maji ya Unesco yazinduliwa, Brasilia, Brazil

Ongezeko la idadi ya watu, kubadilika kwa lisha pamoja na maendeleo yamepelekea kuwepo upungufu wa maji safi duniani.
Serikali zinalazimika kutegemea zaidi usimamizi wa maji safi ili kuhakikisha kuwa afya ya jamii inaimarishwa na kukidhi mahitaji ya idadi ya watu duniani inayoongezeka haraka.
Huo ni moja ya ujumbe uliopo katika tafiti yShirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) la Umoja wa Mataifa (UN) iliyowasilishwa Jumatatu katika kongamano la maji la kimataifa huko Brazil.
Mahitaji ya maji yanaongezeka kwa asilimia 1 kwa mwaka, hata wakati mabadiliko ya tabia nchi, uchafuzi wa hali ya hewa na mmomonyoko wa ardhi unatishia ubora wake na kupatikana kwake.
Lakini mpaka sasa, nchi nyingi zimekuwa zikitegemea usimamizi asilia wa mifumo ya maji uliotengenezwa na mwanadamu, kama vile hifadhi za maji, mikondo ya umwagiliaji na mitambo ya kusafishia maji.
Tafiti hiyo pia imezingatia faida nyingi za “miundombinu” ya maji asilia – kama vile mabwawa, bustani za mijini na shughuli za kilimo endelevu—na imegundua kuwa kuna uwekezaji mdogo sana ambao umeelekezwa katika njia mbalimbali za usimamizi wa maji safi.

voaswahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment