Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 24, 2018

FANYENI TAFITI ZENYE KUINUA ELIMU NCHINI-NZUNDA


 Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda akifunga Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA mjini Morogoro leo,  Kulia kwake ni Odilia Mushi Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya Watu Wazima) Ofisi ya Rais TAMISEMI na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Syston Masanja amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliwakabidhi Taasisi yao (ADEM).


 Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA mjini Morogoro leo


Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Morogoro


....................................................................................
Na Fred J. Kibano

Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tixon Nzunda amefungua leo
Mafunzo ya Uimarishaji Stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK) kwa
wawezeshaji watakaowafundisha walimu wanaofundisha madarasa ya MEMKWA mjini
Morogoro.

Akifungua mafunzo hayo mjini Morogoro, Nzunda amewataka washiriki hao kufanya
weledi, uadilifu, na uwajibikaji lakini pia kufanya tafiti zitakazosaidia kuboreshwa kwa
Sekta ya Elimu nchini pamoja na kubadili fikra zao ili kuleta matokeo makubwa.

“Fanyeni weledi, uadilifu, na uwajibikaji, kusimamia na kufanya tafiti, lakini pia
tunategemea mafunzo haya yawabadilishe mwenendo, tabia, kifikra na kimtizamo ili
muweze kwenda kuhamisha maharifa hayo kwa wengine na baadaye muweze kuleta
mabadiliko makubwa ndani ya sekta ya elimu,”amesema.

Nzunda amewataka washiriki hao kuwa makini na wadadisi wakati wote wa mafunzo ili
walimu watakaopatiwa mafunzo ya madarasa ya Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa
Wasiobahatika (MEMKWA).

“Nitoe wito kwenu washiriki wa mafunzo haya, kuwa makini na wadadisi kwa madazote
zitakazowezeshwa ili nanyi mfikishe maudhui hay ohayo kikamilifu kwa walimu
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA,”amesema.

Nzunda ameyataja moja ya mafanikio ya MEMKWA ni pamoja na mwaka 2012 ilitoa wanafunzi 4170 waliochaguliwa kujiunga na darasa la tano na wengine 1576waliweza kujiunga na masomo ya sekondari.

Aidha, amesema licha ya ongezeko kubwa la watoto wanaoandikishwa darasa la
kwanza, bado idadi ya watoto katika elimu ya mfumo huu usio rasmi (MEMKWA) ni
kubwa ikilinganishwa na msisitizo wa Serikali wa kuifanya Elimu ya Msingi kuwa bure
nay a lazima.

Amezitaja changamoto zinazoikabili Programu ya MEMKWA kuwa ni pamoja na walimu
kukosa umahiri wa kufundisha stadi za KKK, kukosekana kwa mtaala na miongozo ya
kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu, kutokuwepo kwa takwimu sahihi za watoto
walio nje ya mfumo rasmi, kuchelewa kwa malipo ya honoraria kwa walimu wa
MEMKWA, na kukosa umahiri wa upimaji na tathmini ya maendeleo ya kitaaluma kwa
wananfunzi wa MEMKWA.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dk.
Syston Masanja amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliwakabidhi Taasisi
yao (ADEM) kuratibu kazi ya mafunzo ya Wawezeshaji wa Wawezeshaji kuhusu
uimarishaji wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa Walimu wa
wanaofundisha madarasa ya MEMKWA Tanzania Bara na kwamba ‘Global Partnership
for Education chini ya Programu ya LANES ndiyo imefadhili uendeshaji wa mafunzo.

Aidha, amesema anatarajia mafunzo hayo yatafanyika kwa vitendo zaidi na mbinu
mbalimbali ili kuwafanya wanafunzi watakaofundishwa kuweza kufurahia masomo hapo baadae.

“lazima twende zaidi kwa practicals (vitendo), kwa sasa kuna njia nyingi, teknolojia
nyingi ili anayesoma afurahie somo , tunataka mkalete matokeo kule” amesisitiza Dk.
Masanja
Kwa upande wake , Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu (Elimu ya Watu
Wazima) Ofisi ya Rais TAMISEMI, Odilia Mushi  amesema jumla ya wawezeshaji 80 watapatiwa
mafunzo ambao watakwenda kuwapatia mafunzo walimu wapatao 1594 katika vituo
vitatu vya Chuo cha Ualimu Morogoro, Chuo cha Ualimu Tukuyu(Mbeya) na Chuo cha
Ualimu Butimba (Mwanza) lakini pia Maafisa Elimu Mikoa (Elimu ya Watu Wazima na
Elimu Nje ya Mfumo RAsmi) watahusishwa ili kupata uelewa kuhusu mwongozo
ulioboreshwa na kufanya ufuatiliaji.

Aidha, Mushi amesema, Nia ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kama Serikali inataka
wanafunzi wanaochukuliwa kwa mfumo wa MEMKWA wasiwepo ifikapo mwaka 2020
na hivyo wabakie wale tu watakao kuwa ndani ya Mfumo Rasmi wa Elimu.

Mafunzo hayo ya walimu wa MEMKWA baada mafunzo ya siku mbili ya wawezeshaji
yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 26 Machi, 2017 hadi 14 Aprili, 2018 ambapo mada
kadhaa zitatolewa ikiwa ni pamoja na Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu nje ya Mfumo Rasmi, Utekelezaji wa Mtaala ya Elimu ya Msingi kwa watoto walio nje ya Mfumo Rasmi kwa darasa la kwanza na la pili, Maandalizi ya Ufundishaji na Ufundishaji Kiduchu kwa darasa la kwanza na la pili, Utekelezaji wa Mtaala ya Elimu ya Msingi kwa watoto walio nje ya Mfumo Rasmi kwa darasa la tatu na la nne na pia Ufuatiliaji na Tathmini ya Maendeleo ya Elimu nje ya Mfumo Rasmi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment