Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 25, 2018

Askofu: kuna haja ya kuwa na Katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo



Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli basi kuna haja ya kuwa na katiba mpya na si iliyopo sasa.

Askofu Dk Fredrick Shoo alisema hayo baada ya kutoa ujumbe wa Pasaka na kusema kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo ya kweli kwani katiba mpya ndiyo inaweza kuongoza kila raia.

"Katiba iongoze kila raia, utaratibu wa Watanzania kuweza kuishi pamoja na kama tunataka maendeleo ya kweli pasipo Katiba mpya tutakuwa tunajidanganya" alisema Askofu Shoo

Mbali na hilo Askofu Shoo aliweza kuzungumzia mambo mengi kuhusu usalama wa nchi na watu wake na kuonyesha wasiwasi kuwa kuna vitu haviendi sawa kutokana na kuibuka kwa mambo ambayo si utamaduni wa Tanzania, kama watu kupigwa risasi, kuokotwa kwa miili ya watu baharini, kuuwawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment