Mhubiri raia wa Marekani Billy Graham, mmoja wa wahubiri waliopata umaarufu mkubwa duniani katika karne ya 20 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Graham alipata umaarufu mkubwa kama mhubiri wa Kikiristo akihubiri injili sehemu mbali mbali za dunia, kwenye mikutano mikubwa akianzia London mwaka 1954.
Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa alikuwa amehubiria jumla ya watu milioni 210.
Alianza kujitolea kuwa mkiristo akiwa na miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kutakaswa kuwa mhubiri mwaka 1939.
Graham ambaye alikuwa amefanya kaza kama afisa wa mauzo alikuja kuibuka kuwa muungaji mkono mkubwa wa Ukiristo.
Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles.
Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kuwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi kwenye jamii nchini Marekani.
No comments
Post a Comment