Writen by
sadataley
3:15 PM
-
0
Comments
Leone Serikali ya Sierra Leone imetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyoambata na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown imepindukia elfu moja.
Maiti za wahanga wa maafa ya Sierra Leone
Maafisa wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maafa hayo imepindukia elfu moja hususan kwa kutilia maanani mamia ya watu waliotoweka na hawajulikani waliko hadi hii leo.
Takwimu zilizotolewa na waziri wa serikali ya Freetown zinaesema kuwa, hadi sasa zaidi ya watu elfu moja wamethibitika kuwa waliaga dunia kutokana na maporomoko ya udongo ya mji wa Regent.
Awali shirika la Hilali Nyekundu la Sierra Leone limetangaza kuwa watu wasiopungua elfu tatu wamepoteza makazi yao kutokana na maafa hayo ya maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown na kwamba watu wengine 500 hawajulikani waliko.
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga wa maafa ya hayo.
Jeshi la Sierra Leone na timu za uokoaji zinaendelea na kazi ya kutafuta wahanga wa maafa hayo makubwa.
Parstoday
No comments
Post a Comment