Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, August 28, 2017

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesisitiza kusitishwa mashambulizi na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.
Waislamu wa Rohingya wa nchini Myanmar 
Mabudha wenye misimamo mikali wa Myanmar 
Papa Francis ameeleza kusikitishwa na mashambulizi hayo dhidi ya Waislamu wa Rohingya wa nchini Mynamar na kusema kuwa: Watu wote wanapaswa kusaidia ili kufanikisha kukomeshwa mashambulizi na hatua za ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar. 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ameongeza kuwa haki za jamii hiyo ya Waislamu zinapasa kuheshimiwa. Waislamu wapatao 92 wa kabila wa Rohingya wameuawa katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita wanaoishi katika mkoa wa Rakhine huko Myanmar kufuatia kushadidi mashambulizi na ukandamizaji wa jeshi la nchi hiyo.
Mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Mabudha wenye misimamo mikali na wanajeshi wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi hiyo tangu miaka kadhaa iliyopita hadi sasa yamesababisha kuuliwa na kujeruhiwa maelfu ya Waislamu hao na kuwafanya makumi ya maelfu ya wengine kuwa wakimbizi. Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikandamizwa kwa miaka kadhaa sasa huku wakinyimwa haki zao za msingi. 
Parstoday

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment