Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 27, 2017

RC Rukwa azuia Tani 2143 za Madini kuuzwa nje ya Nchi


Katika kasi ya kuhakikisha madini ya watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.

Sakata hilo liliibuka baada ya Mh. Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani  na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.


Usafirishaji wa madini hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.

Wakati Mh. Zelote akiendelea na ukaguzi  katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.

“Sisi tunajuwa kwamba bandari hii inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, Haiwezekani tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials” kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na sio “raw materilas.” Mh. Zelote alisema.

Na kuongeza kuwa Utaratibu uliopo ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe.

Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.

Kwa upande wake afisa wa bandari hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.

IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment