Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 20, 2017

Waziri Mwakyembe ametuma Ujumbe huu

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Dk Harrison Mwakyembe amewashukuru viongozi wote wa Serikali, sekta binafsi, taasisi za Kidini vyombo vya habari na watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke wake.

Linah Mwakyembe amefariki dunia  15 mwaka huu katika hospitali ya Kairuki kwa ugonjwa wa saratani ya titi.

Mwakyembe amesema  kuwa amefarijika sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki kigumu na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kila jambo.

“Mimi na wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na mmetuonyesha  ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi Mungu awabariki sana na asanteni sana”Amesema  Waziri Mwakyembe.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema wananchi wa Mbeya watamkumbuka marehemu  kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo kufundisha jamii kumcha Mungu pamoja na Ujasiriamali uliosaidia wanawake wa Kyela kujiajiri.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment