Wakimbizi kutoka Burundi waliokimbilia nchini Tanzania waanza kurejea nyumabani
Wakimbizi kutoka nchini Burundi waliokimbilia nchini Tanzania na kupewa hifadhi baada ya ghasia kuzuka nchini humo mwaka 2015 wameanza kurejea nchini mwao.
Wakimbizi hao wamenza kurejea nchini Burundi siku chache baada ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kufanya ziara nchini Tanzania.
Rais Pierre Nkurunziza katika ziara yake nchini Tanzania alikutana na rais John Pombe Magufuli ambapo walitoa wito kwa wakimbizi kurejea nyumbani.
Baada ya wito huo kumeonekana makundi ya wakimbizi kuitikia wito huo na kuanza kurejea nchini Burundi.
Kiongozi wa mkoa wa Ruyingi Aloys Ngenzirabona, mkoa ambao unapatikana Mashariki mwa Burundi mpakani na Tanzania amesema kuwa wakimbizi wameanza kurejea kwa wingi mkoani Muyinga, Makamba na Ruyigi.
Kiongozi huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wangi miongoni mwa wakimbizi walioamua kurejea nyumbani hawakutoa taarifa katika ofisi za Umoja wa Mataifa zinazohudumia wakimbizi UNHCR.
Watu 431 000 walilazimika kukimbia nchi wengi wao nchini Tanzania.
Tanzania ilipokea wakimbizi 240 000 huku Rwanda ikiwa na wakimbizi 87 000.
No comments
Post a Comment