Serikali yamwaga fedha kwenye kilimo
Writen by
sadataley
12:00 PM
-
0
Comments
Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imesema tayari imeshapokea fedha za kutosha kutoka serikalini kwa ajili ya kuanza kufadhili miradi mikubwa ya kilimo yenye mwelekeo wa kujenga uchumi wa viwanda.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Francis Assenga amesema maelezo kamili ya namna fedha hizo zitakavyopatikana yataanza kutolewa wakati wa maadhimisho ya sherehe za wakulima maarufu kama Nane Nane ambayo benki hiyo itaadhimisha katika takribani kanda tano nchini.Aidha, Assenga amesema mazungumzo ya jinsi ya kuibua miradi ya kipaumbele kwa kilimo yanayofanyika baina yao na wakuu wa mikoa yamefikia hatua nzuri na kwamba kinachofanyika sasa ni uchambuzi ili kuja na miradi ambayo iwapo itapatiwa fedha italeta matokeo chanya katika mwelekeo mzima wa mnyororo wa thamani katika kilimo.
No comments
Post a Comment