Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 22, 2017

Mawakili wa Lissu wazuiwa kumuona

Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume  

Dar es Salaam. Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema mpaka sasa hajaruhusiwa kumuona mteja wake licha ya kufika Polisi Makao Makuu tangu asubuhi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Julai 21, Karume aliyekuwa na wakili mwingine wa Chadema, Peter Kibatala amesema wameambiwa Lissu hatapelekwa mahakamani kwa sasa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

“Tupo hapa tangu asubuhi, tunaambiwa hatuwezi kumuona kwa sasa, lakini jambo la kushangaza ni kuwa tunaambiwa hatapelekwa mahakamani kwa kuwa uchunguzi haujakamilika ingawa kosa bado halieleweki,” amesema.

Amesema polisi wamewaambia mawakili wa Lissu kuwa hata dhamana kwa leo haitawezekana kwa sababu upelelezi haujakamilika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment