Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 18, 2017

Ma-adimin wa 'Whatsapp group' wapewa onyo kali

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya, Francis Ole Kaparo.

Viongozi wa makundi ya mitandao ya kijamii hasa hasa 'Whatsapp' nchini Kenya wameonywa kujiepusha na kutuma ujumbe zilizokuwa na chuki katika kipindi cha uchaguzi kinachoenda kuanza siku chache zijazo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi Mkuu nchini humo, Francis Ole Kaparo huku akisisitiza kuwa hawawezi kufunga ama kuzuia watu wasitumie mitandao ya kijamii ila wanawataka waitumie kwa uwazi na umakini.

"Waambieni wasimamizi wa makundi ya WhatsApp wanaoruhusu kutumwa kwa ujumbe zenye chuki katika kipindi hiki cha uchaguzi, tunakuja kwa ajili yao,'We will not shut down the internet during elections but it must be used responsibly, tell administrators of WhatsApp groups fanning hate speech, we are coming for them", amesema Kaparo.

Kwa upande mwingine, ni mara ya kwanza leo kwa wagombea wenza wa urais (Makamu wa Rais) nchini Kenya wanakutana ana kwa ana kwenye mdahalo wa kihistoria utakaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Catholic University of Eastern Africa (CUEA) mjini Nairobi.

Wagombea wenza hao ni  Eliud Kariara,  Emmanuel Nzai,  Kalonzo Musyoka,  Miriam Mutua, Moses Marango,Orina Momanyi, Titus Ng'etuny pamoja na William Ruto
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment