Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 27, 2017

Humoud Jumaa Amshukuru Rais Magufuli Kwa Kumpatia Gari La Kubeba Wagonjwa

Na Omary Mngindo, Mlandizi
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa amemshukuru Rais Dr. John Magufuli kwa kumpatia gari jipya kwa ajili ya kubeba wagonjwa.

Jumaa alitoa kauli hiyo muda mfupi kabla ya Waziri wa afya Ummy Mwalimu kumkabidhi rasmi gari hilo lililotolewa na Rais Magufuli huku mbunge huyo akikabidhi magari mawili mapya aliyoyanunua kwa fedha zake lengo kuboresha huduma hiyo kwa wapiga kura wake wanaoishi ndani ya Kata 14 zinazounda jimbo hilo likiwa na vijiji 35.

Alisema kuwa jimbo lake lina changamoto kubwa kuhusiana na suala la usafiri kwa wagonjwa kutoka eneo moja kwenda lingine hivyo alipoona hivyo akaamua kununua magari hayo lengo ni kufanikisha usafirishaji wagonjwa kutoka katika zahanati kwenda vituo vya afya pia kutoka vituo hivyo kupelekwa katika hospitali Teule ya Tumbi au Muhimbili.

“Namshuru sana Mheshmiwa Rais kwa moyo wake, lakini pia nikushukuru nawe Waziri kwa kusimamia hili, gari zilizoingia nchini ni 17 tu nasi tupo wabunge 400 moja kuja hapa si jambo rahisi, siku uliyoniambia unalipeleka Longido nilipatwa na presha, shahidi mke wangu, lakini nakushukuru kwani nilivyokueleza kwamba nimeshawaambia wapigakura ukanielewa na leo umenikabidhi," alisema Jumaa.

Akizungumza na wananchi waliofika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mtongani, Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli katika mambo ambayo imewekea kipaumbele kikubwa katika sekta ya afya na katika kuthibitisha hilo imeongeza bajeti ya fedha katika wizara hiyo lengo likiwa kikidhi mahitaji kwa wananchi.

"Katika mambo ambayo serikali inayoongozwa na Rais wetu mpendwa ni kuhusu suala la afya, amenunua magari, vitanda, magodoro na mashuka vyote hivyo vimeshakabidhiwa katika halmashauri mbalimbali hapa nchini, pia imeboresha huduma za mama na mtoto sanjali na wazee hivyo haitokuwa tayari kuona baadhi ya watumishi wakihujumu juhudi hizo," alisema Ummy.

Aidha amewaonya vikali baadhi ya madaktari na watumishi katika sekta hiyo wenye tabia ya kuwatoza fedha wagonjwa wanaokwenda katika zahanati na vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na kwamba waache mara moja kwani wataobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kazi za kisheria.

Akitoa shukrani kwa Waziri Ummy, Mwenyekiti wa halmashauri Mansour Kisebengo alisema kuwa wamejipanga kuhakimisha hakutokjwepo na utozwaji wa gharama yeyote kwa wagonjwa wataotumia huduma ya usafiri huku akionya kama kuna watu wenye tabia hiyo kuacha mara moja na kwamba wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafanikisha malengo hayo.

Kaimu Mkurugenzi Geda Mmbaga alimweleza Waziri huyo kuwa ofisi yake itawadhibiti baadhi ya watumishi wasio waadilifu na kwamba watawachukulia hatua zinazostahiki lengo likiwa ni kurudisha heshina na nidhamu kazini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment