Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 22, 2017

Simba wataka kufanya maandamano ya amani, Wamechoshwa na TFF


 KUFUATIA sakata la kamati ya katiba, hadhi na wachezaji kuliweka tena mezani suala la Klabu ya Simba kupewa pointi 3 dhidi ya Kagera baada ya kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, wekundu hao wa Msimbazi wametuma barua kwa Kamanda kwa kanda maalum Mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro kuomba maandamano ya amani.

Maandamano hayo amb kwa mujibu wa barua hiyo ya leo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne kuanzia majira ya saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana yakianzia Makao Makuu ya klabu hiyo kuelekea  Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dhumuni kuu la barua hiyo ni kupinga namna Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufanya vitendo na maamuzi ya uonevu kwa Klabu ya Simba huku malalamiko mengi ya msingi wanayopeleka maombi yakiwa hayasikilizwi kwa wakati.

Mbali na hilo ni pamoja na leo, Shirikisho hilo kuamua kumpeleka Msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili ikiwa wanaonyesha nia ya kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asioongelee uonevu unaofanywa dhidi yao.

Barua ya kuomba maandamano hayo ya amani imendikwa na Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva na kutuma nakala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na maandamanio hayo yatapitia katika barabara za Msimbazi, Nyerere na Chang'ombe.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment