Writen by
sadataley
1:04 PM
-
0
Comments
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akizungumza wakati Akifungua Mafunzo ya Ujasiriamali Mkoa wa Mbeya
Meneja
wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede kawataka wanawake wa Mkoa wa Mbeya
kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano
Foundation. Amesema hayo mapema leo jijini Mbeya alipokuwa akifungua
mafunzo ya wanawake 30 juu ya masuala ya ujasiriamali na urembo
yanayoendeshwa ta Taasisi ya Manjano Foundation .
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akiwa Ameambatana na Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Mama Fatuma Kange Pamoja na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser
“Shekha
Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono na
kila mmoja kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kwa kutumia
bidhaa ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake wadogo
kupata mafunzo ili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema
meneja wa SIDO.
Mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser Akizungumza Machache kwenye ufunguzo huo.
Ameongeza
kuwa mbali na Taasisi ya Manjano Foundation kutoa elimu ya ujasiliamali
kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe kuwaunganisha wanawake
hao na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ili kupata mitaji ya
kuanzisha biashara zao.
Mgeni Rasmi akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamamli Mkoa wa Mbeya.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa
wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza
kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa
zilizopo kwenye tasnia ya Urembo.
Aidha
ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake
katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.
Picha na Fullshangwe blog
No comments
Post a Comment