Writen by
sadataley
1:00 PM
-
0
Comments
01: WAJERUMANI WALIVYOSAFISHA KABILA LA WAHERERO
2:WASOVIETI/USSR WALIPOHAMISHA JAMII NZIMA ya WACHECHNYA
3:HAITI:MAUWAJI YA PARSLEY/EL CORTE au (KUKATWA)
Ukabila usikie tu redioni. Hii ilikuwa ni vita ya kikabila. Wadominika
walipanga kuwauwa WaHAITI karibu wote nchini mwao chini ya DIKTETA
Rafael Leonidas Trujillo. Njia pekee ya kumtofautisha Mdominika na
MUHAITI kwa walioleta utata kuwatambua ilikuwa matamshi ya hilo neno/ua
PARSLEY, wahaiti walikuwa hawawezi kulitamka vizuri kutokana na Lugha
yao. Wote walioshindwa waliuwawa kinyama. Kuepusha risasi zisiishe
mapema, Hapa ilikuwa ni Mapanga na marungu asubuhi na mchana.
4:TAIPEI REBELION: CHINA WATU ZAIDI YA 20mil WALIPOTEZA MAISHA.
Hapa ilikuwa ni vita kati ya jamaa aliwaaminisha watu kuwa yeye ni MDOGO
WAKE YESU. Akitawala karibu 1/3 ya nchi yote Hong Xiuquan. Akiongoza
jeshi dhaifu kabisa kwa nia ya kuondoa kamali,uonevu, ndoa za wake wengi
etc, China ilijikuta chini aya vita vya miaka 10 na kuacha raia zaidi
ya 20MIL wakifa na mamia kupotea.
5:UTURUKI DHIDI YA WANAVIJIJI WAASI
baada ya kupiga picha inasadikiwa wote hao waliuwawa na hao wanajeshi
Wanakijiji wa eneo la DERSIM, walipoleta ubishi kuwa chini ya serikali ya UTURUKI badala yake wakang'ang'ania sheria na taratibu zao, Jeshi lilitumwa, Makabila matatu yaliyojisalimisha yaliuliwa wote, Wakina mama na watoto waliokimbilia kwenye Mapango, Yalifunikwa na mawe, moto ukawashwa na wakafa kwa moshi.Inakadiliwa kwa siku moja watu karibu 2MIl waliuliwa na wengine kutekwa.
6: DICTETA Wakirusi STALIN alipoua Mamilioni UKRAIN kwa Njaa.
7:MAUWAJI YALIYOFANYA NA WAZUNGU DHIDI YA WAMAREKANI ASILIA (wahindi wekundu)
Mamilioni ya hawa jamaa waliuliwa bila huruma. Ila hapa tutuzaungumzia
kabila dogo tu la MOQUI katika mji ulioitwa AWATOVI huko ALIZONA.
Wahispania Makasisi walifika wakawalazimisha jamaa kuwa wakristo
wakagoma. Ikabidi liitwe jeshi, maana wakazi waliwachukia wahispania na
wachache waliobadili dini. Wanaume wakiwa kwenye sherehe Walivamiwa na
kuuliwa. Wanaume wote. Wanawake na watoto wakachukuliwa mateka. Wakiwa
njiani wakabishana wawapeleke wapi, wakaamua kuwaua woote ili
kujipunguzia mizigo.
8:Jean Jacques Dessalines alipoigeuza HAITI kuwa taifa la watu weusi 100%
9:VITA VYA BIAFRA - NIGERIA
Tofauti na tanzania tunamakabila mengi yanayopendana, na Nyerere
alisaidia kikubwa, Hii haikuwa hivyo Nigeria. Wanamakabila zaidi ya 300
na yalikuwa karibu karibu kilichosababisha ugomvi mara kwa mara.Tatizo
lilianza pale Kabila/kundi kubwa la IGBO walipojikatia nchi na
kutengeneza nchi yao ya BIAFRA eneo tajiri kwa mafuta. Serikali haraka
ikataka kuwarudisha. Kwa mbinu katili kabisa hata kuzuia chakula na maji
yasielekee BIAFRA. Inasemekana kila siku walikuwa wanakufa watu zaidi
ya 5000 wengi wao IGBO. Watu zaidi ya Milioni 3 walikufa hadi vita
kuisha.
Chanzo: Muungwana Blog
No comments
Post a Comment