Writen by
sadataley
8 years ago
-
0
Comments
Rais Trump ametangaza kuwa hatahudhuria hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wa Ikulu ya White House.
Hafula hiyo kwa kawaida huwavutia wageni mashuhuri, wanasiasa na waandishi wa habari. Tangazo lake limetolewa juma moja baada ya Rais kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya mashirika ya habari.
Kwa kawaida hafula hiyo ya kila mwaka ya White House hutoa nafasi kwa waandishi wa habari na Rais kusahau tofauti zao kwa muda.
Hata hivyo uhusiano kati ya waandishi na Rais Trump umezorota kwa majuma machache yaliyopita.
Rais amewasema baadhi ya waandishi wa habari na taasisi wanazofanyia kazi kama habari bandia na kuwataja kama maadui wa wa Marekani.
Mnamo Ijumaa, Ikulu ya White House iliwafungia nje waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa Rais. Miongoni mwa waliofungiwa nje ni CNN, New York Times pamoja na BBC.
Waandalizi wa hafula hiyo wamesema kuwa itaendelea na uhuru wa vyombo vya habari utapewa kipao mbele kulingana na Katiba ya Nchi.
BCC
No comments
Post a Comment