Writen by
sadataley
8 years ago
-
0
Comments
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers Tanzania Gospert Katunzi akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo mashine ya uchunguzi wa uwoni baada ya kufungua kambi ya uchunguzi wa macho katika kijiji cha Uroa Mkoa Kusini Unguja. (kushoto) Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba ambae alifanikisha kambi hiyo.
Abdulrahaman Abdalla wa Kitengo cha macho cha Mikunguni akimfanyia uchunguzi wa macho mwanafunzi Hafsa Suleiman Ali katika kambi ya uchunguzi wa macho Kijiji cha Uroa inayoendeshwa na Lions Club ya Dar es salam.
Mratibu wa Lions Club ya Dar es salaam Mustasir Gulamhussein akimuhoji Bibi Saumu Pandu Simai namna anavyoweza kuona baada ya kumpima na kumpatia miwani kutoakana na matatizo aliyonayo.
Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo waliofika kufanyiwa uchunguzi wa macho na kupatiwa dawa na miwani kwa waliobanikia na matatizo ya uwoni.
Baadhi ya wananchi waliofika Skuli ya Uroa kuchunguzwa afya ya macho wakimsikiliza mbunge wao Bangwanji Mensuria Mshamba.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Lions Club ya Dar es salaam, wanaoendesha kambi ya uchunguzi wa macho, wakiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba na Waziri Mahmoud Thabit Kombo.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
No comments
Post a Comment