Writen by
sadataley
1:25 PM
-
0
Comments

Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (kulia) akiongea jambo wakati akiwaeleza wananchi na
wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Nyamagongo Wilaya ya Rorya
kuhusu utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya III. Shule hiyo ni miongoni
mwa maeneo ambayo yatafikiwa katika mradi wa REA awamu ya Tatu. Wengine
wanaofuatilia ni Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa Mhandisi Amos
Maganga, (katikati) Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rorya, Sospeter Kswahili
(wa kwanza kulia). Wengine ni Mtaalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini
Mhandisi Emmanuel Yesaya na Mkandarasi wa Kampuni ya Angelica
International.

Afisa Uhusiano na Huduma za Jamii kwa
Wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), James Vesso, akitoa
elimu kuhusu Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha
Muriaza Kata ya Muriaza Wilaya ya Butiama wakati wa Ziara ya Waziri wa
Nishati na Madini kijijini hapo. Kifaa hicho hakihitaji mtandao wa umeme
katika nyumba.

Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa
Mhandisi Amos Maganga, akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa
Nishati na Madini wananchi wa Nyamagongo ambapo Waziri na wataalam wa
REA na TANESCO wameeleza kuhusu utekelezaji wa REa Awamu ya Pili na ya
Tatu. Wengine ni Mameneja wa TANESCO, Wilaya ya Rorya na Mkoa wa Mara,
na Wataalam kutoka REA na TANESCO.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha
na viongozi wa Mkoa, wakimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo (kulia) wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kukagua
miradi ya REA awamu ya II na kueleza mipango ya Serikali kuhusu
utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini
la Taifa (STAMICO), Mhandisi Hamis Komba, akiwaeleza wachimbaji wadogo
kuhusu shirika hilo kuridhia kutoa sehemu ya eneo lake la Buhemba kwa
ajili ya wachimbaji kufanya shughuli za uchimbaji madini.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo akitoa rambirambi kwa baadhi ya wazazi ambao mmoja wa
wachimbaji wadogo alifariki katika ajali ya kifusi iliyotokea katika
mgodi eneo la Buhemba, Mkoani Mara.
Sehemu ya wananchi wa wananfunzi katika
eneo la Nyamagongo Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara wakifuatilia mkutano wa
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, hayupo pichani
Naibu Mhariri wa Gazeti la Jamhuri
Jackton Manyerere (wa pili kulia) akiongea jambo wakati Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa heshima
katika Kaburi la Baba Mzazi wa Manyerere., Jakcton Nyambereka Nyerere
aliyefariki dunia tarehe 19/2/2017/. Wa kwanza kulia ni Mhariri wa
gazeti la Mtanzania Kulwa Keredia. Kushoto ni baadhi ya waandishi kutoka
vyombo mbalimbali vya habari. Waziri alifika kuhani msiba wa wahariri
hao Manyerere na Keredia wakati wa ziara yake Wilayani Butiama.
No comments
Post a Comment