Writen by
sadataley
1:21 PM
-
0
Comments

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya ELimu, Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa kwa
furaha na mwenyeji wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt.
Akinwumi Adesina ofisini kwake jijini Abidjan, Ivory Coast

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha ripoti
ya Kizazi cha Elimu kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt.
Adesina

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt.
Akinwumi Adesina na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt, Makthar Diop
pembezoni mwa mkutano huo.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa za
ELimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina alipomtembelea katika Makao
Makuu ya Benki hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu
Kikwete amewasilisha kwa Rais Adesina ripoti ya Kamisheni ya Elimu na
kuwasilisha rai ya Kamisheni hiyo ya kuiomba Benki ya Maendeleo ya
Afrika kusaidia nchi za Afrika kugharamia miradi na mageuzi ya sekta ya
elimu katika nchi zao. Rai hiyo ya Kamisheni inatokana na ripoti kubaini
kuwa misaada na mikopo inayotolewa kwa sekta ya elimu imekuwa ikishuka
ikilinganisha na zile zinazotolewa kwa miradi ya afya na miundombinu.
Kamisheni inaamini kuwa bila kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu,
watoto wapatao milioni 223 duniani (takribani milioni 160 wakiwa Afrika)
watakosa fursa ya kupata elimu ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Rais Adesina ameupokea
ujumbe huo na kusema kuwa takwimu zilizoibuliwa na Ripoti ya Kamisheni
‘zinakatisha tamaa na pia zinatoa changamoto’. Rais Adesina ameahidi
kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika itaitizama Ripoti hiyo na mapendekezo
yake na iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Kamisheni katika kutafuta
majawabu ya changamoto zilizopo katika elimu barani Afrika. Amesema kuwa
Benki yake inatambua kuwa kuwekeza katika vijana na nguvu kazi ya
Afrika ndio jawabu la maendeleo ya uhakika huko mbeleni.
Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu
amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Makhtar Diop
pembezoni mwa mkutano wake na Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika. Ziara ya Rais Mstaafu nchini Ivory Coast itahitimishwa kwa
kukutana na Rais wa Ivory Coast Mhe. Alassane Ouattara.
No comments
Post a Comment