Writen by
sadataley
9 years ago
-
0
Comments

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni akiwasili katika Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo
Vingunguti Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Kampuni za Bakhresa Bw. Salim Aziz.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe.
Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika
viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo
Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini
Dar es Salaam.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni
akiangalia namna Juisi ya Azam inavyotengenezwa alipofanya ziara katika
Kiwanda hicho leo Jijini Dar es Saalam. Kulia ni Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage.

Rais wa Uganda Mhe.Yoweri
Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika
viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es
Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya
Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni
ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri
Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya
Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda
Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya
Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni
na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es
Salaam.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya
kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa
Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam
kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine
Mahiga.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara
baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food
Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo
Vingunguti Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi
la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara
baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food
Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo
Vingunguti Jijini Dar es Salaam

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya
Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kumaliza ziara katika
Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo
Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini
Dar es Salaam
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
No comments
Post a Comment